Tuesday 20 December 2011

WANANCHI TUWE MAKINI NA BIDHAA ZILIZOPITWA NA MUDA WAKE WA WATUMIZI

BIDHAA ZILIZO EXPIRE ZAKAMATWA ZANZIBAR



Na Fatma Kassim, Maelezo Zanzibar 20/12/2011
BODI ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar imefanikiwa kukamata tani mbili za tende ambazo zimepitwa na wakati katika maghala mawili Mjini Zanzibar
Tende hiyo imegunduliwa ikiuzwa na wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) katika maeneo ya Darajani kwa bei ya shilingi Mia tano kwa Nusu kilo na kupigwa Muhuri wa bandia kuwa inamalizika muda wake wa matumizi mwaka 2012.
Ukamatwaji wa tende hiyo unatokana na Operesheni ya kukagua bidhaa katika Mabucha mbali mbali ya Nyama kulikofanywa na na Bodi hiyo leo katika maeneo mbali mbali ya Mjini Zanzibar.
Mrajis wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar, Dk Burhan Othman Simai amesema kuwa baada ya kuwakamata  wafanyabiashara hao waliwapeleka kituo cha polisi na kuweza kusaidia kuonesha sehemu walikoipatia tende hiyo.
Amesema Maghala yaliyogundulika ni pamoja na Ghala la Malindi linalomilikiwa na Ali Amour Mohammed na Ghala la Kwa Haji Tumbo linalomilikiwa na Mohammed Abdalla Rashid.
Kwa mujibu wa Maelezo ya Mrajis amesema Tende hiyo ambayo imekwisha muda wake wa Matumizi inatarajiwa kuangamizwa hivi karibuni ambapo gharama za uangamizaji wa bidhaa hiyo itatolewa na wamiliki wa bidhaa hiyo.
Aidha katika Operesheni hiyo BODI ya Chakula Dawa na Vipodozi imebaini kasoro mbali mbali zikiwemo zile zinazohatarisha afya ya binadamu.
Katika kupambana na hali hiyo amesema hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuyafungia baadhi ya mabucha na kuwafungulia mashataka wauzaji 36 wa nyama katika maeneo mbali mbali ya Unguja.
Dk Burhan amefahamisha kuwa hatua nyengine itakayochukuliwa ni kufanya operesheni maalum na kubwa ambayo itafanyika hivi karibuni ambayo itakagua mabucha yote, sehemu za kuuzia bidhaa za mifugo pamoja na machinjio kwa upande wa Unguja na Pemba.
Ukaguzi huo utajumuisha Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Jeshi la Polisi.

Habari hii ni kwa hisani ya 

No comments:

Post a Comment