Wednesday, 14 December 2011

MDAU AADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANGANYIKA KWA KUUZA BIDHAA ZA KITANZANIA KWENYE MAGULIO YA ULAYA

Wengine wakiwa wanaadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania kwa sherehe, siasa nyingi, vigelegele, mivinyo na vinubi, mimi na mtoto wangu tulikuwa tanaadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa nchi yetu Tanzania kwa kuuza na kutangaza bidhaa za Kitanzania kwenye magulio ya wenzetu ulaya. Niliona  kuliko kwenda Pub, au kusikiliza hotuba za kusadikika ni bora kwenda kuuza bidhaa za rafiki yangu "Fundinguo"  kwenye masoko ya wenzetu kama wao wanavyouza bidhaa zao nchini mwetu. Wadau wenzangu, Kamwe Tanzania hatutaweza kuendelea kiuchumi au kijamii  kama hatutajitahidi kuzalisha bidhaa zetu wenyewe kwa ajili ya matumizi  yetu ya ndani  na pia kwa ajili ya kuuza nchi za nje. Ni muhimu pia kujenga utamaduni wa kutumia vitu vilivyozalishwa na kutengenezwa nchini mwetu  kwa jasho letu, mikono,akili, nguvu  na rasirimali zetu zilizozagaa kwenye kila kona ya nchi yetu kuliko kutegemea bidhaa kutoka china. Kwa kufanya  hivi ajira zitaongeza  kwa vijana na watu wote, kipato kitaongezeka, uchumi wetu utakua na Tanzania itaendelea.  Achana na  maneno ya siasa , hii dhana  ni  halisi  kwa maendeleo ya nchi wala haina  chegachenga  kama maneno meeeengi ya wanasiasa wanaotaka ubunge  au Uraisi ili walipize visasi kwa maadui zao, wamiliki migodi, washibishe matumbo yao, walipe madeni yanayowakabili na kadhalika.

Mdau, 
Shilingi Shop Japan.

Pichani ni Mdau wenu akipigwa na Jua kwenye  kwenye moja ya Magulio siku ya Uhuru wa Tanzania
Tukiuza Kanga Bags kutoka kwa Fundinguo  

Dogo kachoka anataka "Obento"

Tunajadiliana Tufanyeje, 
Mdau,
Shilingi Shop Japan

1 comment:

  1. Mimi ni Mtanganyika hakuna nchi iliyopewa uhuru na kuitwa Tanzania ilikuwa ni Tanganyika 1961 na Zanzibar ilipata uhuru wake 1963.
    Mkuu usilitupe taifa letu la Tanganyika.


    "The name Tanzania derives from the names of the two states Tanganyika and Zanzibar that united in 1964 to form the United Republic of Tanganyika and Zanzibar, which later the same year was renamed the United Republic of Tanzania.[8]"

    ReplyDelete